Manchester United ipo Tayari Kumuuza Bissaka

Klabu ya Manchester United inaelezwa kua ipo kwenye mpango wa kumuuza beki wake wa kulia Aaron Wan Bissaka kama ofa nzuri itakuja ndani ya klabu hiyo ndani ya dirisha hili kubwa.

Manchester United ina mpango wa kupitisha fagio ndani ya klabu hiyo hivo itauza baadhi ya wachezaji ambao wanaona hawana nafasi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo wanawapiga bei kama Bissaka, Huku wengine wakiondoka kwa uhamisho huru.manchester united

Beki huyo mwenye asili ya Congo raia wa kimataifa wa Uingereza alikua sokoni toka msimu uliomalizika lakini hakuna timu iliyofikia bei ambayo klabu hiyo ilihitaji, Lakini mwaka huu Man United wako tayari tena kumuweka sokoni kwa timu ambayo itafanikiwa kufika kiwango walichoweka watamuachia beki hiyo.

Klabu ya Manchester United imewaeka sokoni wachezaji wengine kadhaa ukiachana na Wan Bissaka wachezaji hao ni kama Mason Greenwood, Jadon Sancho, pamoja na Harry Maguire hawa ni wachezaji ambao timu zikifika bei ambayo klabu hiyo inahitaji basi ni wazi wachezaji hao watatimka kwenye timu hiyo.

Acha ujumbe