Casemiro Rasmi Kukosekana Wiki Kadhaa

Kiungo wa klabu ya Manchester United Carlos Casemiro imethibitika atakua nje ya uwanja kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha ambayo ameyapata katika mchezo wa juzi dhidi ya Newcastle.

Casemiro atakua nje ya uwanja kutokana na majeraha ya misuli ya paja ambayo ndio sababu ya kukosekana uwanjani kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil.casemiroKiungo huyo alipata majeraha wiki kadhaa nyuma akiwa na timu ya taifa ya Brazil na akakosekana uwanjani kwa wiki takribani mbili, Lakini atakua nje ya uwanja tena baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Newcastle.

Klabu ya Manchester United imekua kwenye kipindi kibaya sana hivi karibuni kutokana na matokeo mabaya, Lakini pia wachezaji wake kupata majeraha mara kwa mara jambo ambalo linaelezwa kuendelea kuchochea matokeo mabaya ya klabu hiyo.casemiroKiungo Casemiro msimu huu anaonekana kua na msimu mbaya kutokana na majeraha ambayo anakumbana nayo kwasasa tofauti na msimu uliomalizika, Ambapo alikua moja ya wachezaji walifanya vizuri sana ndani ya kikosi cha Manchester United.

Acha ujumbe