Casemiro Hakieleweki Man United Apata Majeraha Tena

Kiungo wa klabu ya Manchester United Carlos Casemiro mambo yamemuaendea upande ndani ya klabu hiyo msimu huu, Kwani inaelezwa amepata majeraha tena baada ya kurejea jana kutoka majeruhi.

Casemiro alirejea jana katika mchezo  dhidi ya Newcastle United lakini akitolewa baada ya mapumziko, Huku kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag akithibitisha kiungo huyo alitoka kwajili ya majeraha aliyoyapata.casemiroKiungo huyo inaelezwa atakosekana katika mchezo wa Jumamosi mapema ambao watakipiga ugenini dhidi ya Fulham katika dimba la Craven Cottage, Hili linakua pigo lingine kwa mashetani wekundu.

Klabu hiyo msimu huu imekua ikiandamwa na majeraha kwa kiwango kikubwa wachezaji wamekua wakipishana kwenye majeraha, Kwani akipona mmoja wanaumia wawili jambo ambalo limekua likichangia timu hiyo kupata matokeo mabaya.casemiroTaarifa rasmi ya Casemiro atakosekana kwa muda gani haijawekwa wazi bado lakini inafahamika mchezo wa JUmamosi dhidi ya Fulham ataukosa akiungana na wachezaji wengine kama Lisandro Martinez,Tyrell Malacia, Luke Shaw na Raphael Varane.

Acha ujumbe