Yanga Yarejea Kileleni Kwa Mbinde

YANGA iliibuka na ushindi wa bao 1-0 Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Jana usiku, ushindi ambao walitumia nguvu kubwa sana kupata kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe ulivyokuwa. Unatabiri ni timu gani itabeba ubingwa, Leo Simba anakipiga na Tabora Utd beti mechi hii ikupe mkwanja wa kutosha kutoka Meridianbet.

 

yanga

Bao pekee la ushindi lilifungwa na kiuongo Mudathir Yahya dakika ya 86 akitumia vema pasi ya mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage aliyeingia kipindi Cha pili kuchukua nafasi ya Joyce Lomalisa.

Mudathir na Kibabage wote wawili walitokea benchi kipindi cha pili ambapo Dodoma Jiji walikuwa wanakaribia kupata pointi moja bahati mbaya mpango wao ukakwama dakika za mwisho za mchezo huo.

Mbinu ya Dodoma Jiji ilikuwa ni kujilinda zaidi na kushambulia kwa kushtukiza Jambo ambalo halikuwapa matokeo. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Sasa Yanga inarejea nafasi ya kwanza ikiwashusha Azam FC mpaka nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya tatu.

Ni pointi 34 imekusanya baada ya kucheza mechi 13 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 31 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 26 baada ya kucheza mechi 11. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.