KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Salum Abubakari ‘Sure Boy’ muda wowote atafanyiwa operesheni ya bega ikiwa ni baada ya kupata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar. Ligi kuu ya NBC inaendelea kwa michezo kadhaa, Yanga yupo Dar na Simba yupo Mwanza unaweza kubashiri mechi hizi zote kupitia Meridianbet zina odds kubwa. Bonyeza hapa kuona nafasi yako ya ushindi wiki hii.
Mchezo huo ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera ambao ulimalizika kwa suluhu ambao ulimuacha na jeraha baya la bega amabalo linaweza kumuweka nje kwa takribani wiki mbili kwa mujibu wa taarifa za madaktari wa klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa, kiungo huyo alipata majeraha makubwa ambayo yalimsababishia ashindwe kuendelea na mchezo huo. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiungo huyo atafanyiwa vipimo maalum na madaktari wa timu hiyo, kabla ya kufanyiwa oparesheni ambayo huenda ikamuweka nje ya uwanja zaidi ya mwezi mmoja.
“Sure Boy yupo chini ya uangalizi hivi sasa wa madaktari ambao wanatarajiwa kumfanyia vipimo kabla ya kufanyiwa operesheni ya bega.
“Hiyo ni baada ya bega lake kuonekana limepata jeraha kubwa, hivyo hivi sasa yupo chini ya uangalizi huku akiendelea na matibabu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Akizungumzia hilo Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema: “Ni kweli Sure Boy alipata majeraha makubwa ya bega, hivyo anatarajiwa kufanyiwa operesheni.”


