Singida Yamalizana na Nyota Wawili wa Yanga

KLABU ya Singida Fountain Gate imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha usajili wa David Bryson na Dickson Ambundo wote kutoka katika timu ya Yanga.

Ambundo alitangazwa kuachana na Yanga wiki iliyopita baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo. Upande wa Bryson yeye hadi juzi Jumatatu bado alikuwa hajatangazwa lakini anaonekana akiwa Singida.singidaMakamu Rais wa Singida ambaye ni Mbunge wa zamani John Kadutu alisema wanakwenda kufanya makubwa msimu ujao, kwa sababu wamefanya usajili wa maana kwa wachezaji wa ndani na nje ambao wana uwezo.

Kuhusu nyota hao wa Yanga Kadutu alifunguka kuwa: “Kimsingi siyo wachezaji hao tu ambao watu wanawajua, lakini kuna wale wachezaji 12 wakigeni nao usajili wake umefanyika kwa asilimia kubwa.singida“Hatutaki kwenda kushindana, ila tunataka kushinda kwenye kila mashindano ambayo tunakwenda kushiriki msimu ujao.”

Acha ujumbe