Ferlan Mendy Yupo Sana Madrid

Beki wa kushoto wa  klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ufaransa Ferlan Mendy inaelezwa bado yupo yupo sana ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.

Beki Ferlan Mendy anatarajiwa kuongeza mkataba wa miaka mitatu ambapo ataendelea kuwepo klabuni hapo mpaka mwaka 2027, Beki huyo amekua kwenye kiwango bora sana klabuni tangu ajiunge na timu hiyo licha ya ukosoaji ambao amekua akiupata ndani ya klabu hiyo.ferlan mendyBeki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa amekua akihusishwa kutimka klabuni hapo baada ya Real Madrid kuhusishwa na beki wa klabu ya Bayern Munich Alphonso Davies, Lakini mpaka sasa inaonekana mchezaji huyo ataendelea kusalia ndani ya mabingwa hao wa ulaya.

Klabu ya Real Madrid ipo kwenye mkakati wa kuongezea mikataba wachezaji wake muhimu ndani ya kikosi hicho, Huku Ferlan Mendy akiwa miongoni mwao kwani mpaka sasa makubaliano yameshafikiwa kilichobaki ni kusaini mkataba huo mpya kiuhalisia beki huyo amestahili mkataba mpya klabuni hapo kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha.

Acha ujumbe