Sababu Nne Zinazowapeleka Simba Uturuki

SIMBA wanatarajia kwenda zao Uturuki kwenye kambi ya maandalizi yao ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya ndani ikiwemo Azam Sports Federation (FA).

Uongozi wa Simba unataka timu ipate utulivu zaidi wakati wa maandalizi na ndiyo maana wametafuta nchi ya Uturuki ambayo wanaamini itakuwa na utulivu ambao wanahitaji.SimbaSasa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahemed Ally ametoa sababu nne ambazo zimefanya wao wachague kwenda Uturuki licha ya kuwa kuna nchi nyingine ambazo wangeweza kupata utulivu.

Ahmedy Ally alisema: “Kuhusu kambi ya Simba Uturuki. Maswali ni mengi kwanini mnaenda Uturuki si mngebaki tuu kama wenzenu

“Jibu ni kwamba hela ya kwenda Uturuki ipo tuu sio mpaka tuuuze jezi. Pili timu ya inayoshiriki Super League lazima iwe tofauti na wengine.Simba“Tatu timu ya 9 kwa ubora Afrika lazima ifanye maandalizi sehemu kubwa kubwa. Nne wachezaji wetu wana hadhi ya Uturuki na Ulaya. Halafu watu wa Uturuki wamefurahi kusikia tunaenda wamesema tumelipa heshima taifa lao.”

Simba wanatarajia kuondoka siku za hivi karibuni kwenda Uturuki kwa ajili ya pre-season hiyo.

Acha ujumbe