Wachezaji Simba Waitwa Haraka Kambini

simba

Habari kutoka ndani ya Simba SC zinasema kuwa, mabosi wa Simba wameamua kuwaita wachezaji wote ili kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya safari ya nje ya nchi zikitajwa Afrika Kusini au Uturuki itakapowekwa kambi ya maandalizi ya msimu mpya kulingana na maelekezo ya Roberto Oliveira. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Kundi la kwanza la wazawa litakalopimwa kuanzia Jumatatu, linahusisha wachezaji 12 waliopo kikosi cha sasa akiwamo nahodha John Bocco, Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Kibu Denis, Ally Salim, Ahmed Feruzi Teru, Israel Mwenda, Mzamiru Yasin, Jimmyson Mwanuke, Nassor Kapama, Habib Kyombo na Mohamed Mussa.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Kundi la pili litakalojumuisha wachezaji 10 wageni na kipa Aishi Manula aliyetoka kufanyiwa upasuaji hivi karibuni Afrika Kusini, litafanyiwa vipimo Jumanne likiwa na Moses Phiri, Joash Onyango, Sadio Kanoute, Jean Baleke, Saido, Chama, Henock Inonga, Peter Banda na Pape Ousmane Sakho.

“ Haya ni maandalizi ya kuanza safari ya kwenda kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya, kocha kataka wote wafanyiwe vipimo mapema kisha zianze taratibu za safari ya kwenda kuweka kambi ya msimu mpya, kisha naye atajumuika wiki chache zijazo sambamba na nyota wapya walisajiliwa na watakaosajiliwa, ” alisema mmoja wa vigogo wa klabu hiyo aliyeomba kuhifadhiwa jina.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Kigogo huyo alisema wito huo unajumuisha wachezaji wote bila kujali kana kuna waliopo kwenye hesabu za kupewa ‘Thank You’, kwa vile hadi sasa hakuna maamuzi mengine yaliyofanyika baada ya kutemwa kwa nyota tisa Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Beno Kalolanya na Gadiel Michael.

Wageni waliopigwa chini hadi sasa ni Wanigeria Nelson Okwa na Victor Akpan, Mghana Augustine Okrah na Mohamed Ouattara kutoka Burkina Faso, na Ismael Sawadogo, huku Joash Onyango na Peter Banda wakitajwa wapo kwenye mazungumzo kutokana na kuwa na mikataba inayowabana.

Onyango inaelezwa ameomba kuondoka Msimbazi, huku Peter Banda akikomaa akitaka kuvunjiwa mikataba kama hayupo kwenye Mipango ya klab kwa Msimu ujao na sio kutolewa kwa Mkopo. Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Acha ujumbe