Miquissone Kuvuna Milioni 95 Simba

Zipo tetesi juu ya kuwa winga wa zamani wa Simba Luis Jose Miquissone yupo mbioni kurejea Simba, baada ya kukosa nafasi kwenye klabu yake ya sasa ya Al- Ahli.

Chanzo cha ndani kutoka Simba kinasema mshahara wa nyota Miquissone kama atarejea Simba utakuwa ni asilimia 100 ya ule ambao anavuna Al-Ahli kwa sasa ambao ni milioni 95 za Kitanzania na usajili ukiwa ni takribani milioni 800.miquissoneMtoa taarifa huyo ambaye yupo jirani na uongozi wa juu wa Simba aliyeomba hifadhi ya jina alisema: “Miquissone yupo tayari kurudi Simba na amekubali kuja kuvaa tena jezi ya timu yetu. Lakini ametoa sharti la kulipwa asilimia 100 ya mshahara ambao analipwa Misri.

“Mshahara wake ni milioni 95 na ameuambia uongozi hitaji lake na mwekezaji wetu Mo Dewji amesema hakuna shida juu ya hicho anachokitaka ingawa kuna viongozi wanaona kama hela nyingi.”

Kwa upande wa Simba, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally alisema kuwa: “Suala la usajili linakwenda kuwa hadharani muda siyo mrefu. Watu wataona balaa kuna vifaa vya maana.miquissone“Nchi hii itatikisika, ndiyo maana sitaki kusema au kuongelea kuhusu nani anakuja na nani amepata kiasi gani cha usajili. Watulie, kazi ndiyo kwanza imeanza.?

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu ya Al Ahly kwasasa inazingatia chaguzi zingine lakini bado nafasi iko wazi kwa Simba na wanawapa kipaumbele kwenye dili hilo.

Acha ujumbe