Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino amesema klabu yake inapaswa kuanza kufunga mabao katika michezo yao, Kwani mpaka sasa wanacheza vizuri lakini wanapaswa kufunga magoli sasa ili kushinda mchezo.
Klabu ya Chelsea imeshindwa kufunga mabao katika michezo yake miwili yake mitatu ya mwisho, Hili jambo ambalo kocha Pochettino anaona kama ndio tatizo la msingi kwa upande wao kwasasa.
Klabu ya Chelsea msimu huu imeendelea kua na kiwango cha chini kwa msimu wa pili mfululizo, Huku makocha wakiendelea kuja tofauti tofauti ndani ya timu hiyo.
Kocha Pochettino anaamini kama watajitahidi kuhakikisha wanafunga magoli katika michezo yao ya mbeleni itawasaidia, Kwani kikawaida hwezi kushinda mchezo wa mpira wa miguu bila kufunga bao hivo ni wazi wanapaswa kufunga magoli.
Klabu ya Chelsea ni moja klabu iliyofanya usajili mkubwa mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza tangu msimu uliomalizika, Lakini mpaka sasa muendendo wa klabu hiyo hauonekani kua kwenye uelekea mzuri licha ya kocha wa klabu hiyo kueleza wanacheza vizuri na wanachohitaji ni kufunga magoli.

