Arda Guler Apata Majeraha Tena

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Real Madrid zinaeleza kua kiungo kinda wa klabu hiyo mwenye kipaji kikubwa Arda Guler ameripotiwa kupata majeraha ndani ya klabu hiyo.

Arda Guler ameonekana mazoezini ndani ya klabu hiyo mapema jana na ilielezwa tayari yupo fiti kwajili ya kuanza kuitumikia klabu hiyo, Lakini taarifa ya leo inaeleza kinda huyo atakua nje ya uwanja kwa muda wa takribani wiki tatu.arda gulerKiungo huyo alipata majeraha akiwa katika mechi za kujiandaa na msimu huku akiwa hajafanikiwa kucheza mechi yeyote ya ushindani ndani ya klabu ya Real Madrid, Wakati huu ambapo ilidhaniwa kua kiungo ndio amerejea uwnajani lakini mambo yameenda tofauti.

Kiungo huyo mwenye kipaji kikubwa ambaye anatabiriwa makubwa ndani ya klabu hiyo ni wazi ataendelea kukosekana ndani ya timu hiyo kwa muda mwingine zaidi ambapo inakadiriwa wiki tatu mpaka nne anaweza kua nje ya uwanja kutokana na tatizo la misuli.arda gulerArda Guler alifanikiwa kuonesha ubora mkubwa sana ndani ya klabu ya Fenerbahce licha ya umri wake mdogo wa miaka 18, Lakini alifanikiwa kupata nafasi kwenye kikosi cha timu jambo ambalo liliwavutia Real Madrid kumsajili ambapo kwasasa amekua akiandamwa na majeraha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.