Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amemtabiria makubwa mchezaji wake wa zamani ndani ya timu hiyo Xabi Alonso ambaye kwasasa anaifundisha klabu ya Bayern Leverkusen ya Ujerumani.
Kocha Ancelotti anasema kiungo huyo ana uelewa mkubwa wa mpira wa miguu na ndi sababu kiungo anafanya vizuri kwasasa ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen.Kocha huyo anaamini kingo huyo siku moja ataweza kuja kua kocha wa klabu ya Real Madrid, Hii inatokana na kitu kikubwa ambacho anakiona ndani ya Xabi Alonso ambapo mpaka sasa anafanya vizuri ndani ya Bayern Leverkusen.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Real Madrid kwasasa anafanya vizuri katika ligi kuu ya Ujerumani ambapo anakinoa kikosi cha Bayern Leverkusen ambacho mpaka sasa kikosi hicho kinaongoza ligi kuu ya Ujerumani, Hii inaendelea kudhihirisha kua ni kwa namna gani kocha huyo anaweza kuja kufanya makubwa.Kocha Carlo Ancelotti anaamini mchezaji wake huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid ana uwezo wa kuwa kocha mkubwa zaidi, Kwani mpaka sasa ameshaonesha uwezo wake ndani ya Bayern Leverkusen na mpaka sasa taarifa zinaeleza kua Alonso anaweza kua ajaye wa Real Madrid.