Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameweka wazi kiungo wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Croatia hana mpango wa kuondoka klabuni hapo.

Kiungo Luca Modric amekua akihusishwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na vilabu vya nchini Saudia Arabia, Lakini kocha Ancelotti amebainisha kua kiungo huyo alishaamua kusalia klabuni hapo kwakua aliongeza mkataba mpya.ancelottiWachezaji mbalimbali kwasasa barani ulaya wamekua wakihusishwa na kujiunga na vilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia na hiyo ikiwa ni kutokana na ofa kubwa ambazo vilabu hivo vimekua vikitoa kwa wachezaji.

Kiungo Luca Modric amesaini kandarasi ya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo licha ya vilabu mbalimbali kuulizia huduma yake na atakuwepo klabuni hapo mpaka mwezi Juni mwaka 2024 ambao ndio utakua ukomo wa mkataba wake.ancelottiKocha Ancelotti anasema anajua kiungo huyo hana furaha kwakua hachezi mara kwa mara na ni jambo la kushangaza Modric kutokucheza, Lakini amesema atapata dakika za kucheza na atawasaidia ndani ya msimu huu.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa