Joao Felix Hataki Kubaki Atletico

Winga wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ureno Joao Felix hataki kubaki ndani ya klabu hiyo na hiyo ni baada ya rais wa klabu hiyo kutoa kauli hiyo.

Rais wa klabu ya Real Madrid Enrique Cerezo amefunguka kua winga Joao Felix hana mpango wa kusalia ndani ya viunga Wanda Metropolitano na hapo hilo linafahamika hivo wanasubiri klabu ambayo itaweka ofa kwa mchezaji huyo ili waweze kumuuza.Joao FelixWinga huyo amekua akionesha kutohitaji kubakia ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu kwani wiki kadhaa alinukiliwa akisema anapenda kujiunga na mabingwa wa soka nchini Hispania klabu ya Barcelona.

Klabu ya Atletico iliamua kumtoa kwa mkopo winga huyo wa kimataifa wa Ureno kwenda  klabu ya Chelsea mwezi Januari hiyo ikielezwa kua hakua anafurahishwa na na namna kocha Diego Simeone anamchezesha kwenye timu hiyo. Joao FelixMchezaji Joao Felix amekua akihusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali mpaka sasa barani ulaya lakini hakuna klabu ambayo imefanikiwa kutuma ofa kwa klabu ya Atletico Madrid, Mchezaji ameonesha nia yake ya kujiunga na Barcelona lakini tatizo mabingwa hao wa Hispania wanapitia ukata inawezekana ndio sababu hawajapeleka ofa mpaka sasa.

 

Acha ujumbe