Baada ya kumpata Karim Benzema mabingwa wa ligi kuu nchini Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League klabu ya Al-Ittihad sasa wamehamishia nguvu kwa winga wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah wakiwa wanamuhitaji kwenye timu yao.
Mabingwa Al-Ittihad inaarifiwa wamejiandaa kutuma ofa kwa klabu ya Liverpool kwajili ya kumsaini mchezaji huyo ili aweze kuungana na wachezaji wengine kuongeza nguvu klabuni hapo ndani ya msimu huu na kuhakikisha wanaendeleza ubabe kwenye ligi hiyo.Klabu hiyo imeelezwa kua imeandaa ofa kubwa kwa mshambuliaji Mohamed Salah kama atakubali kujiunga na klabu hiyo, Wachezaji wengi wanaoondoka barani ulaya inatokana na ofa kubwa ambazo vilabu hivo kutoka Saudia vinaweka mezani.
Vilabu kutoka Saudia Arabia vimeendelea kua tishio kwa vilabu barani ulaya kwani wamekua wakiweka ofa kubwa ambazo wachezaji wengi wanashindwa kuzikataa kutoka kwa wachezaji wenye umri mkubwa mpaka sasa wamehamia kwa vijana wadogo.Klabu ya Liverpool wao wanaelezwa hawana mpango wa kufanya mazungumzo na klabu yeyote juu ya Mohamed Salah na wakimuona mchezaji huyo kama mchezaji asiyeuzika, Hivyo mpaka sasa Al-Ittihad wanapaswa kua na ushawishi mkubwa zaidi kwa Liverpool.