SIMON MSUVA AGOMBEWA ALGERIA

WAKATI Bongo, stori ya Simon Msuva ikiwa ni kuhusishwa na mapacha wa Kariakoo Yanga na Simba, habari ni tofauti nchini Algeria ambako inadaiwa kuwa Msuva ameziingiza vitani klabu mbili za ligi kuu.

Ripoti ya AfricanFoot na Eric Ndagijimana inasema, Msuva anawaniwa na JS Kabylie na Cs Costantine zote za ligi kuu, Eric anadai kuwa Kabylie ndio walikuwa wa kwanza kutupa ndoano na baadae Cs Costantine wakafuatia.SIMON MSUVALicha ya klab ya JS KABYLIE ya Algeria kuonyesha nia kubwa ya kuipata huduma ya kiungo Mshambulaiji Mtanzania Simon Msuva,

Huenda Msuva akaungana na Cs Costantine na kuipata huduma ya mchezaji huyo na ikifahamika kuwa ndio wameweka ofa bora, kubwa na nzuri kuliko hata Js Kabylie,

Mpaka kufikia muda huu bado Simon Msuva hajatoa maamuzi ya Juu ya wapi atasaini kandarasi ya kuwatumikia licha ya klab ya Js Kabylie kuwa ndio walimualika kwenda Algeria kwa mazungumzo.SIMON MSUVAEric ameongeza kuwa Jumamosi ya wiki, ndiyo itakuwa siku ambayo itafahamika wapi atacheza nyota huyo wa zamani wa Yanga, Wydad Casablanca, Difaa El Jadida na nyinginezo

Acha ujumbe