SIMBA WAWAJIBU YANGA KWA JEURI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa, wao malengo yao msimu huu ni kushinda mechi zote watakazocheza kwenye ligi na mashindano mengine, huku wakiweka rekodi ya kuwa timu isiyofungika.

Hayo yalikuwa maneno ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally. Mwamba huyo maarufu kama msemaji wa Caf alisema, watashinda mabao mengi kwenye kila mchezo na hawataruhusu bao lolote kwenye mechi hizo.SIMBA“Tunasikitika kuwa, tumecheza mechi mbili za ligi mpaka sasa na kufunga mabao sita tu na kuruhusu mabao mawili. Hili ni jambo ambalo hatuwezi kulifurahia.

“Kwa namna ambavyo timu yetu ilivyo na wachezaji bora na wakali zaidi barani Afrika, ilipaswa tuwe tumefunga mabao mengi sana na kutoruhusu bao lolote. Tumeshinda mabao sita na kuruhusu mawili.

“Kocha wetu na wasaidizi wake, wanakwenda kurekebisha hilo, tunataka kuwa klabu iliyofunga mabao mengi na kufungwa mabao machache,” alisema Ahmed.SIMBASimba waliwachapa chuma 4-2 Mtibwa Sugar pale Manungu Morogoro kwenye mchezo wa kwanza na kisha kuwachapa Dodoma Jiji FC mabao 2-0 kwenye mechi ya pili iliyochezwa Uwanja wa uhuru.

Acha ujumbe