Winga wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ureno Joao Felix ameingia kwenye rada za kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag katika dirisha hili la usajili.
Joao Felix ambaye amerudi kwenye klabu yake ya Atletico Madrid akitokea klabu ya Chelsea ambapo alikua kwa mkopo wa nusu msimu, Kocha Ten Hag anataka kumuongeza mchezaji kama sehemu ya maboresho ya kikosi chake.
Ten Hag anaripotiwa kua mshabiki mkubwa wa winga huyo wa kimataifa wa Ureno na anamuhitaji kwenye kikosi chake kwakua anaona ni mchezaji ambaye anaweza kuongeza kitu kikubwa ndani ya klabu hiyo katika eneo la ushambuliaji.
Joao Felix imekua ikielezwa kua aina ya mpira wa klabu ya Atletico Madrid chni ya kocha Diego Simeone imekua haimfai na anafaa akicheza zaidi kwenye timu ambayo inacheza mpira wa kushambulia na sio wa kuzuia kama wa kocha Simeone.
Kocha Ten Hag yeye inaelezwa kua atahitaji saini ya winga huyo kwa mkopo wa msimu mzima kutokea klabu ya Atletico Madrid, Huku upande wa Joao Felix unakielezwa hauna tatizo na suala hilo zaidi wakitegemea maamuzi ya klabu ya Atletico.

