Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameeleza kua klabu hiyo haina mpango wa kusajili beki mwingine wa katikati baada ya beki Eder Militao kupata majeraha.

Beki Eder Militao anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kupata majeraha, Ambapo ilitarajiwa klabu hiyo itasajili beki mwingine lakini kocha Ancelotti amesema mabeki waliokua nao kikosini kama Alaba, Nacho, na Rudiger.ancelottiKlabu ya Real Madrid sasa itakua na mabeki watatu wa katikati baada ya Militao kupata majeraha yanayokadiriwa kua yatakua ya muda mrefu, Hivo wengi waliamini kua kukosekana kwa beki huyo kutasababisha kua klabu hiyo itasajili beki mwingine wa katikati.

Real Madrid imekumbwa na majeraha kwa wachezaji wake wawili muhimu ambao watakua nje ya uwanja kwa muda mrefu ambao ni Eder Militao na golikpa Thibaut Coutois, Lakini kwa upande wa golikipa Madrid wametafuta mbadala lakini kwa beki Militao wanaonekana hawana mpango wa kusajili.ancelottiKocha Ancelotti amedhihirisha kua klabu hiyo haina mpango wa kusajili beki mwingine wa kati, Huku mashabiki wengi wa Real Madrid wakiamini kua klabu hiyo inapaswa kusajili beki mwingine wa katikati ambae atakua na ubora wa kuvaa viatu vya Eder Militao.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa