Mbappe Atakuwepo Mchezo Ujao wa PSG

Mshambuliaji wa klabu ya PSG Kylian Mbappe anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha klabu hiyo kuelekea mchezo ujao wa timu hiyo dhidi ya klabu Tolouse.

Mbappe amerejea kwenye klabu ya PSG rasmi wiki hii baada ya kutokuepo kwenye klabu hiyo kwa kipindi chote ambacho klabu hiyo ilikua inafanya maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa michuano mbalimbali ambayo klabu hiyo ilikua inashiriki.MbappeMshambuliaji huyo alikua anakaribia kutimka klabuni hapo na klabu hiyo ilikubali kumuweka sokoni baada ya kukataa kusaini mkataba mpya, Lakini mchezaji huyo na PSG walifikia makubaliano ambayo yalimrudisha mchezaji huyo kwenye sehemu ya timu hiyo.

PSG wameonekana kukubaliana na mchezaji huyo na kukubali kusalia ndani ya timu hiyo baada ya kua na mvutano wa muda mrefu baina ya mchezaji huyo na mabingwa hao wa soka nchini Ufaransa.MbappeMshambuliaji Kylian Mbappe kurejea kwake ndani ya klabu hiyo ni wazi sasa dili lake la kujiunga na klabu ya Real Madrid limekufa ndani ya msimu huu, Kwani mwanzo iliripotiwa hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo tena lakini kurejea kwake kwenye timu kumeleta taswira mpya na kuonesha yupo kwenye mipango ya timu hiyo.

Acha ujumbe