Kcha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameweka wazi mahusiano baina yake na beki wa kimataifa wa Ufaransa Raphael Varane ambaye anakipiga ndani ya klabu hiyo.
Ten Hag ameweka wazi kua hakuna tofauti yeyote baina yake na beki huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Huku akisisitiza zinazoendelea ni tetesi tu na hazina ukweli.
Taarifa zilikua zinaeleza kua beki Raphael Varane ameingia kwenye mzozo na kocha huyo kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Jambo ambalo kocha huyo amesema sio kweli ni tetesi tu ambazo watu wanaziibua.
Beki Raphael Varane anaelezwa kutofurahishwa na kutopata nafasi ndani ya kikosi hicho haswa beki Johny Evans kupata nafasi mbele yake ni jambo ambalo halijamfurahisha beki huyo.
Kocha Erik Ten Hag ameendelea kusisitiza hakuna kibaya kinachoendelea baina yake na beki Raphael Varane, Zaidi ukiwa ni ushindani wa namba baina ya wachezaji wake kama inayoonekana leo atacheza Varane, kesho Evans na wakati mwngine anacheza Maguire.

