Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kua klabu hiyo hiyo haina hatia mpaka sasa licha ya kutuhumiwa na kesi 115 kupitia masuala ya matumizi ya fedha.
Guardiola anasema anajua watu wengi wanataka wafungiwe kama ambavyo vilabu vingine vinafungiwe baada ya kuvunja ya sheria ya FFP akiitaja Everton, Lakini kocha huyo amesisitiza kua klabu hiyo haina hatia.
Kocha huyo amesema kesi yao na ya klabu ya Everton ambao wamepokonywa alama kumi wiki iliyopita ni kesi mbili tofauti kabisa, Lakini akiwataka watu kutulia kwakua mpaka sasa hawana hatia na wanasubiri maamuzi ya kamati.
Manchester City walituhumiwa kwa tuhuma 115 zinazohusiana na uvunjaji wa taratibu za matumizi ya fedha tangu mwaka jana, Hivo wengi walitarajia wapate adhabu lakini mpaka sasa hawajaadhibiwa japo vilabu vingine vinaadhibiwa.
Kocha Guardiola anasema anajua fika kabisa wengi wanataka kuona wanaadhibiwa, Lakini hawaezi kuadhibiwa mpaka mashtaka yakamilike jambo ambalo mpaka sasa halijatokea hivo ni wazi hawana hatia kwasasa na watu wanaotoka waadhibiwe watulie.

