Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag ameweka wazi kua golikipa namba moja wa klabu hiyo Andre Onana atakua fiti kukipiga dhidi ya klabu ya Everton Jumapili hii.
Onana alipata majeraha akiwa anaitumikia timu yake ya taifa ya Cameroon wiki iliyomalizika, Wengi wakitarajia kukosekana katika mchezo dhidi ya Everton wikiendi hii lakini imekua tofauti.Golikipa huyo licha ya kutokuanza vizuri ndani ya klabu hiyo msimu huu lakini amekua moja ya mchezaji muhimu ndani ya klabu hiyo, Hivo kama angekosekana Jumapili ingekua pengo kubwa ndani ya klabu ya Man United.
Kocha Erik Ten Hag amesema golikipa huyo amekua akifanya mazoezi na wenzake kwa siku kadhaa nyuma, Hivo inaonekana golikipa huyo atakipiga katika michezo ijayo ya klabu hiyo kwakua yupo fiti.Klabu ya Manchester United mbali na Onana kua fiti lakini klabu hiyo imepokea urejeo wa beki wake wa kushoto Luke Shaw ambaye alikua nje ya uwanja kwa taktibani mwezi mmoja, Hivo klabu hiyo itakua imerejesha nguvu kuelekea mchezo wao dhidi ya Everton Jumapili.