Onana Amkingia Kifua Garnacho

Golikipa wa klabu ya Manchester United Andre Onana amemkingia kifua winga wa klabu hiyo kinda Alejandro Garnacho baada ya chapisho alililoweka kwenye mitandao ya kijamii.

Winga Garnacho aliweka chapisho lilimjumuisha yeye na golikipa Andre Onana huku akiweka imoji za gorrila, Ambapo ilitafsiriwa kama kitendo cha kibaguzi alichokifanya winga ambapo kipa huyo amemtetea Garnacho.onanaGolikipa huyo amendika kupitia mitandao yake ya kijamii “Watu hawawezi kuchagua kile ninachoweza kuchukizwa nacho, Garnacho alimaanisha nguvu na hili halikupaswa kwenda mbali”onanaChama cha soka nchini Uingereza FA inaelezwa imeanza kuchunguza chapisho la Alejandro Garnacho kama linahusisha aina yeyote ya ubaguzi, Japo golikipa wa klabu hiyo ameonekana kuja hadharani kumtetea mchezaji mwenzake na kueleza hakua analenga kufanya ubaguzi wa aina yeyote.

Winga Garnacho alipandisha chapisho hilo baada ya golikipa Andre Onana kuchomoa mchomo wa penati dakika za mwisho na kuhakiksha Man United inapata alama tatu ambapo chapisho hilo lilionekana na kupongeza, Lakini kitendo cha kuambatana na imoji ya gorrila ndio iliyoleta sintofahamu.

Acha ujumbe