Benzema Ashangazwa na Ronaldo

Mshambuliaji wa klabu ya Al Ettihad Karim Benzema ameshangazwa na ubora wa mchezaji mwenzake wa zamani wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo kutokana na ubora anaouonesha.

Benzema anasema ubora ambao unaoneshwa na Ronaldo kwenye umri wa miaka 38 ni jambo la kushangaza sana, Kwani wengi wanaamini kufunga magoli kwenye ligi kuu ya Saudia ni rahisi jambo ambalo sio la kweli.BenzemaMshambuliaji huyo wa Al Ettihad inayoshiriki ligi kuu ya Saudia Arabia amesema kiwango cha Ronaldo ni cha kushangaza kwani mpaka sasa ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi mwaka 2023 tena akiwa na umri wa miaka 38.

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo amekua na mwaka mzuri sana tangu ajiunge na klabu ya Al Nassr mwezi Jnauari mwaka huu, Kwani ameonesha ubora mkubwa sana ndani ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia.BenzemaCristiano Ronaldo kuanzia mwezi Januari mwaka huu ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 38 akishindana na vijana kama Mbappe na Haaland, Jmabo ambalo limemfanya Benzema kuona kua Ronaldo ni wa kipekee na anastahili kuitwa mchezaji bora wa muda wote.

Acha ujumbe