Declan Rice Aendelea Kuwanyamazisha

Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Declan Rice anaendelea kuwanyamazisha wale waliokua wanapinga kiwango cha pesa alichosajiliwa ndani ya klabu hiyo.

Kundi kubwa la mashabiki lilionesha wazi kua kiungo Declan Rice hana thamani ya kiasi cha Euro Milioni 105 ambacho kilitumika kumsajili kutoka ndani ya klabu ya Westham United wakiamini hakustahili thamani hiyo.declan riceKiwango ambacho anakionesha nahodha huyo wa zamani wa Westham ndani ya klabu ya Arsenal ni kama anawafunga mdomo wale wote ambao walikua wanapinga thamani ya usajili wake kutokana na ubora ambao amekua akionesha klabuni hapo.

Declan Rice mpaka ameonesha kua alistahili kiwango kikubwa cha pesa kwenye usajili wake na hiyo ni kutokana na namna ambavyo anacheza ndani ya timu hiyo, Kwani anaonesha utofauti mkubwa kwenye safu ya kiungo ya timu hiyo.declan riceSafu ya kiungo ya klabu ya Arsenal imeonekana kuimarika kwa kiwango kikubwa baada ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza kujiunga na timu hiyo, Haswa kipindi ambacho kiungo Thomas Partey amekua nje kwa majeraha ya mara kwa mara.

Acha ujumbe