Kiungo wa klabu ya PSG ambaye yupo kwa mkopo klabu ya Rb Leipzig inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Xavi Simons ameendelea kuwasha moto ndani ya klabu hiyo.

Xavi Simons amefanikiwa kufungua akaunti yake ya mabao katika ligi ya mabingwa ulaya jana baada ya kufunga bao katika ushindi wa mabao matatu kwa moja walioupata Rb Leipzig jana.xavi simonsKiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 20 tu amekua na mwendelezo wa kiwango bora tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea klabu ya PSV Eindonhoven ya nchini kwao Uholanzi.

Kiungo huyo licha ya umri wake mdogo lakini amekua akionesha uwezo mkubwa kila siku ndani ya klabu hiyo jambo ambalo linaifanya klabu ya Rb Leipzig kutamani kumbakiza klabuni hapo jambo ambalo sio jepesi.xavi simonsXavi Simons amekua moja ya wachezaji waliohusika kwenye mabao mengi ndani ya klabu ya Rb Leipzig msimu huu, Huku pia akiweka rekodi jana ya kua mchezaji mdogo wa kimataifa wa Uholanzi kufunga bao kwenye michuano ya ulaya tangu alipofanya Arjen Robben mwaka 2003.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa