Guardiola: De Bruyne Bado Muda Wake wa Kurejea

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameeleza kua kiungo wake fundi klabuni hapo Kevin de Bruyne bado muda wa kurejea uwanjani japo anaendelea vizuri.

Guardiola amesema kua Kevin de Bruyne anaendelea vizuri baada ya kupata majeraha, Lakini bado sio muda sahihi wa yeye kurejea uwanjani na kusema hawatalazimisha kiungo huyo kurejea uwanjani.guardiolaKiungo Kevin de Bruyne alipata majeraha ya enka ambayo yamemueka nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili, Lakini taarifa zinaeleza kiungo huyo anaendelea vizuri na yupo mbioni kurejea dimbani.

Kocha Pep Guardiola amesema aina ya majeraha ambayo ameyapata kiungo huyo sio ya kulazmisha kurudi uwanjani haraka, na kueleza watasubiri mpaka madaktari wakubaliane na Kevin de Bruyne kua ni upi muda sahihi wa kiungo huyo kurejea dimbani.guardiolaKiungo Kevin de Bruyne tangu akosekane katika kikosi cha Manchester City pengo lake limeonekana kwa kiasi kikubwa, Kutokana na kukosekana kwa kiungo ambaye ameziba pengo lake ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe