Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameeleza kua kinda wa klabu hiyo Arda Guler atapewa muda wa kucheza tu na haina haja ya kuharakisha kumpa nafasi ya kucheza ndani ya timu hiyo kipindi hichi ambacho ametoka kwenye majeraha.

Kocha Ancelotti anajua lazima kijana huyo lazima awe anahuzunika kutopata nafasi ya kucheza, Lakini anachojua Arda Guler atapata nafasi ya kucheza tu muda wake ukifika.ancelottiKiungo Arda Guler hajafanikiwa kucheza mchezo hata mmoja akiwa ndani ya uzi wa Real Madrid tangu ametua klabuni hapo, Hiyo ikisababishwa zaidi na majeraha ambayo yamekua yakimuandama mara kwa mara tangu amefika klabuni hapo.

Ilitazamiwa kua Arda Guler huenda angepata dakika katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya uliopigwa Jumatano ambapo Real Madrid ilikua inacheza na Sporting Braga, Lakini bado kijana huyo hakupata nafasi ya kucheza.ancelottiKocha Carlo Ancelotti anasema haina haja ya kuharakisha kumchezaesha Arda Guler kwakua ni kijana mdogo na ana muda mrefu ndani ya klabu hiyo, Huku akisema anamsapoti mchezaji huyo kwakua anajua ana kipaji kikubwa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa