Kocha wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Italia Carlo Ancelotti amefanikiwa kupindua rekodi ya kocha Sir Alex Ferguson na kua kocha aliyeshinda michezo mingi kwenye ligi ya mabingwa ulaya.
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson ndie alikua kocha anaeongoza kwa kushinda michezo mingi kwenye ligi ya mabingwa ulaya akiwa na michezo 115na Ancelotti amefanikiwa kuvuka na kufikisha michezo 116.Baada ya ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya Sporting Braga Don Carlo alifanikiwa kuivuka rekodi ya Sir Alex Ferguson ambayo imedumu kwa takribani miaka 10 sasa.
Kocha huyo ambaye amepita vilabu mbalimbali barani ulaya na amepata ushindi huo katika vilabu mbalimbali kama Juventus, Ac Milan, Chelsea, PSG, Napoli, Bayern Munich, na klabu yake ya sasa Real Madrid.Kocha Carlo Ancelotti licha kuweka rekodi ya kua kocha aliyeshinda michezo mingi ta ligi ya mabingwa ulaya, Lakini pia ndio kocha anaeongoza kwa kutwaa taji hilo akiwa ametwaa mataji manne ya ulaya akiwa na vilabu vya Ac Milan na Real Madrid kila klabu akitwaa mara mbili.