Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amezungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu zao Man United na kuzua mjadala baada ya kuonekana kumtetea kocha wa Man United Ten Hag.
Pep Guardiola wakati anazungumza na wanahabari alionekana wazi anahitaji kocha Erik Ten Hag apewe muda wa kutosha na kuacha afanye kazi yake na ataweza kuiweka klabu ya Man United juu.Kocha huyo wakati akijibu swali la muandishi lililomtaka kocha huyo huyo wa Man City kuelezea fomu ya Man United kwasasa inayoonekana kua mbovu “Mechi tisa tu, Man United wanaweza kushinda mechi nne,tano, sita mfululizo na wakifanya hivyo watakua juu, Watoe muda, na wamuache kocha afanye kazi yake”
Klabu ya Manchester United imeanza msimu huu vibaya kwani mpaka sasa imeshapokea vipigo mara nne kwenye ligi kuu ya Uingereza, Huku wakifungwa michezo miwili kwenye ligi ya mabingwa ulaya hivo ikapelekea kuibua minong’ono kua kocha huyo hafai.Kocha Pep Guardiola bado aliendelea kusisitiza tatizo kua Man United likitokea jambo linatazamwa sana, Lakini hiyo haiondoi kua klabu hiyo inapaswa kumpa kocha huyo muda wa kufanya kazi yake akiamini anaweza kuwarudisha kwenye ubora wao.