Guardiola: Messi Anastahili Ballon Dor zaidi

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kua staa wa zamani wa klabu ya Barcelona Lionel Messi ndio anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon Dor.

Guardiola wakati anahojiwa mapema leo alitoa kauli ambayo inaashiria kua yupo upande wa mchezaji wake wa zamani Lionel Messi mbele ya mshambuliaji wake wa sasa ndani ya klabu ya Manchester City Earling Halaand katika tuzo ya Ballon Dor.guardiolaKocha huyo alipohojiwa alisema ” Kila siku nasema Ballon Dor imegawanyika sehemu mbili moja kwa Messi na upande mwingine ni kwa wachezaji wengine waliobaki, Haaland anapaswa kushindwa kwasababu tulibeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja na alifunga magoli mengi, Lakini Messi ameshinda kombe la dunia”

Kocha huyo alienda mbali kwa kusema kwa kuonesha kua anampa nafasi kubwa Messi kushinda tuzo hiyo baada ya kusema kua msimu mbaya kabisa wa Messi ni msimu bora kwa wachezaji wengine kupitia kauli hii inaonesha Guardiola yupo upande wa Messi.guardiolaMchezaji Lionel Messi na Earling Haaland wapo kwenye nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon Dor zinatarajiwa kutolewa ndani ya mwezi huu, Hii inatokana na ubora ambao wachezaji wameuonesha kwa mwaka mmoja uliopita.

Acha ujumbe