Harry Kane Aendelea Kuzifumania Nyavu Bundesliga

Harry Kane anasema anahisi yuko nyumbani Bayern Munich baada ya kufunga bao lake la 18 la Bundesliga msimu huu.

 

Harry Kane Aendelea Kuzifumania Nyavu Bundesliga

Bayern walitawala pambano lao la jana usiku huko FC Cologne lakini walikuwa na bao pekee la Kane dakika ya 20 kuonyesha kwa juhudi zao.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham Kane mwenye miaka 30, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 18 katika mechi 12 za kwanza kwenye ligi kuu ya Ujerumani.

Harry Kane Aendelea Kuzifumania Nyavu Bundesliga

Nahodha huyo wa Uingereza alisema: “Ninajisikia vizuri. Ninahisi niko nyumbani hapa. Kila mtu amenikaribisha vyema kuanzia kwa wachezaji, wafanyakazi, klabu, mashabiki na ninataka tu kuwalipa kila ninapoingia uwanjani.”

Tuna wachezaji wazuri karibu nami ambao wananitengenezea nafasi, kwa hivyo lazima nihakikishe niko mahali pazuri kwa wakati ufaao. Ninajisikia vizuri kwenda kwenye kila mchezo. Najua nitapata nafasi kwenye mchezo. Alisema Kane.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Harry Kane Aendelea Kuzifumania Nyavu Bundesliga

Harry Kane alifunga bao pekee la ushindi kwa Bayern Munich dhidi ya FC Cologne. Katika mashindano yote, Kane amefunga mabao 22 katika mechi 17 tangu kuwasili kwake kwa pauni milioni 86.4 mwezi Agosti.

Aliongeza: “Ulikuwa mchezo mzuri sana kwetu leo. Watu wengine hutazama matokeo na wanaweza kutarajia zaidi kidogo. Lakini ulikuwa mchezo mzuri kutoka kwa kila mtu. Tungeweza kufunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza pekee.”

Alama tatu zinawapeleka vijana wa Thomas Tuchel kileleni kwenye msimamo kabla ya safari ya Bayer Leverkusen dhidi ya Werder Bremen Jumamosi. Leverkusen watarejea nafasi ya kwanza kwa ushindi wao wenyewe.

Harry Kane Aendelea Kuzifumania Nyavu Bundesliga

Bayern watarejea dimbani Jumatano watakapoikaribisha FC Copenhagen katika Ligi ya Mabingwa.

Mabingwa hao watetezi wa Bundesliga tayari wamejikatia tiketi ya kuingia hatua ya 16 bora huku wakiwa wamesalia na michezo miwili katika Kundi A.

Mechi yao inayofuata ya ligi inakuja watakapowakaribisha Union Berlin Uwanja wa Allianz Arena mnamo Desemba 2.

Acha ujumbe