Manchester United Yatakata Tuzo za Mwezi Epl

Klabu ya Manchester United imetakata kwenye tuzo za mwezi za ligi kuu ya Uingereza ambapo wamefanikiwa kutwaa tuzo mbili kwenye tuzo za mwezi Febuari.

Wachezaji wawili wa klabu ya Manchester United wamefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Febuari mshambuliaji Rasmus Hojlund, pamoja na kiungo kinda Kobbie Mainoo ambaye ameshinda goli bora la mwezi.manchester unitedMshambuliaji Rasmus Hojlund amekua na mwezi mzuri ndani ya Febuari kwani alifanikiwa kufunga kwenye michezo minne mfululizo ndani ya mwezi huo akiwa amefunga jumla ya mabao sita.

Kiungo Kobbie Mainoo yeye alifanikiwa kunyakua tuzo ya goli bora la mwezi baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya klabu ya Wolverhampton katika ushindi wa mabao manne kwa matatu.manchester unitedKlabu ya Manchester United imeweza kutakata ndani ya mwezi Febuari kwani katika tuzo zinatolewa ndani ya mwezi wamenyakua tuzo mbili, Huku wakikosa tuzo moja ambayo ni za kocha wa mwezi ilibebwa na kocha Mikel Arteta wa Arsenal.

Acha ujumbe