Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kinatarajiwa kushiriki michuano ya Copa America baada mwezi wa sita kimetangazwa leo na nyota kadhaa wa kikosi hicho wakitemwa wachezaji hao ni kama Casemiro, Gabriel Jesus, na Richarlison.
Wachezaji hao wameachwa kwenye kikosi hicho kutokana na kushuka kwa ubora ambao wamekua nao kipindi cha nyuma, Hiyo ikiwa ni sababu kubwa zaidi inayotajwa kupelekea nyota hao kutemwa kwenye kikosi cha timu hiyo.Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimezingatia zaidi wachezaji wanaofanya vizuri kwenye klabu zao na sio ukongwe historia ya kuwahi kufanya vizuri kwenye timu ya taifa jambo ambalo limefanya wachezaji kama Casemiro, Gabriel Jesus, na Richarlison.
Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichotangazwa leo ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Ederson Man City, Allison Becker Liverpool, Bento Athletico- Pr Mabeki Beraldo PSG, Marquinhos PSG, Danilo Juventus, Wendell Fc Porto, Yan Couto Girona, Gabriel Magalhaes Arsenal, G. Arana Athletico MG Viungo Andreas Perreira Fulham, Dougals Luiz Aston Villa, Lucas Paqueta Westham, Bruno Guimaraes Newcastle, Joao Gomes Wolves, Washambuliaji Endrick Palmeiras, Gabriel Martinelli Arsenal, Rodrygo Real Madrid, Evanilson Fc Porto, Savinho Girona, Raphinha Bracelona, Vinicius Jr Real Madrid.Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kilichoitwa kinaonekana kutengenezwa na vijana wengi wadogo na sura ngeni zikiwa nyingi, Hii kupelekea wachezaji wakongwe kama kina Casemiro kukatwa kichwa kuelekea michuano ya Copa America baada mwezi wa sita ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo ni Argentina.