Wachezaji wawili wa klabu ya Manchester United kiungo Carlos Casemiro na beki Lisandro Martinez wana uwezekano mkubwa wa kucheza mchezo wa jumapili katika mchezo dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs.
Wachezaji hao wawili walikua wanaandamwa na majeraha kwa muda sasa wamefanikiwa kurejea katika uwanja wa mazoezi kwa takribani wiki moja sasa na wako tayari kwa mchezo wa Jumapili.Kocha Erik Ten Hag leo amethibitisha uwepo wa wachezaji Casemiro na Lisandro Martinez kuwepo sehemu ya kikosi kitakachocheza Jumapili dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs katika mchezo utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.
Kurejea kwa wachezaji hao ni wazi itaongeza uimara wa kikosi cha Manchester United kuelekea mchezo huo mgumu dhidi ya Tottenham, Lakini pia katika michezo mingine itakayofuata na hiyo ni kutokana na ubora wa wachezaji hao.Kiungo Casemiro na beki Lisandro Martinez walikua wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Manchester United msimu uliomalizika wakati wanamaliza nafasi ya tatu na kutwaa taji la Carabao Cup, Hivo kurejea kwao ni wazi unakwenda kuimarisha kikosi hichi kwa kiwnago kikubwa sana.