Haaland Kuikosa Newcastle Kesho

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amethibitisha mshambuliaji wake namba moja Earling Haaland atakosekana katika mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Newcastle United.

Haaland anaendelea kukosekana katika michezo ya Manchester City kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama mchezaji bora na mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliomalizka.haalandMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway amekua akiandamwa na majeraha siku za hivi karibuni, Jambo ambalo limefanya klabu yake ya Manchester City kuyumba haswa kwenye eneo la ushambuliaji ikionekana wazi wanaikosa huduma yake kwa kiwnago kikubwa.

Mbali na mshambuliaji Earling Haaland lakini kocha Pep Guardiola pia amethibtisha kukosekana kwa beki wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uingereza John Stones ambaye nae amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi ndani ya klabu hiyo.haalandKlabu ya Manchester City msimu huu wamekua wakiandamwa na majeraha kwa kiwnago kikubwa haswa kwa wachezaji wake muhimu, Ikiwa ni moja ya sababu za klabu hiyo kuonekana kutetereka msimu huu tofauti na misimu kadhaa nyuma ambayo walikua kwenye ubora mkubwa.

Acha ujumbe