Benchika Aipata Simba Aitakayo, Mjiandae Kisaikolojia.

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Abdelhack Benchika amesema kuwa Kwa Sasa hana wasiwasi Kwa kuwa ameshaipata timu ambayo alikuwa anaitaka. Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

BENCHIKA sIMBA, &Fredy

 

Simba imewapa mapumziko ya siku 10 mastaa wa timu hiyo baada ya kutoka kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 iliyofika fainali na kufungwa bao 1-0 na Mlandege, lakini kocha mkuu, Abdelhak Benchikha ni kama amewatega kiaina wachezaji wapya waliosajiliwa kupitia dirisha dogo.

Mastaa wapya waliosajiliwa na Simba ni viungo washambuliaji Saleh Karabaka kutoka JKU na Ladack Chasambi (Mtibwa Sugar), kiungo wa mkabaji Msenegali Babacar Sarr na mastraika wawili Mgambia Pa Omar Jobe na Muivory Coast Freddy Michael Kouablan aliyeongoza kwa ufungaji huko Zambia akifunga mabao 14 na asisti nne katika mechi 16 za Ligi Kuu nchini humo.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Kocha Benchikha alisema timu hiyo ilihitaji ongezeko na mabadiliko ya wachezaji kwenye dirisha dogo lililopita, hivyo mastaa waliosajiliwa wanahitaji kuziba moja kwa moja mapengo yaliyokuwepo na kuhakikisha timu inafanya vizuri.

β€œTulihitaji mabadiliko na kuongeza watu, waliosajiliwa sasa ni jukumu lao kuonyesha umuhimu wao ndani ya timu. Tunataka kufanya vizuri katika kila michuano tunayoshiriki hivyo kila mchezaji anahitajika kuonyesha kwanini yupo Simba,” alisema Benchikha.

β€œTunaendelea kujenga timu itakayokuwa na ushindani na kucheza soka la kuvutia, tutakaporejea naamini tutatengeneza kikosi imara zaidi.”

Beki na kocha zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo β€˜Julio’ alisema wachezaji wapya wamebeba matumaini makubwa hivyo hawapaswi kuwaangusha.

β€œMchezaji anaposajiliwa anakuwa anategemewa kufanya makubwa zaidi, hivyo ndivyo ilivyo na kwa hao wa Simba hivyo wakipata nafasi wanatakiwa kuhakikisha wanaonyesha ubora na faida kikosini. Binafsi siwezi kutoa maoni ya moja kwa moja bali nawapa muda niwaone kwanza,” alisema.Simba inatarajia kuingia kambini Jumatano, wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika zitakazoendelea mwezi ujao.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.