Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saidoo Ntibanzokiza ‘Saido’ amegomea mkataba wa mwaka mmoja alioandakiwa na Uongozi wa Klabu ya Simba huku akiutaka Uongozi wa Simba SC kumpa mkataba wa miaka miwili.
Ntibazonkiza ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao imebakisha miezi sita ya kuendelea kubakia Simba SC, ambayo imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao msimu huu.Kiungo huyo alijiunga na Simba SC wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita, akitokea Geita Gold ambako alisaini mkataba wa miezi sita kabla ya kutua Msimbazi,
Zipo baadhi ya timu zinatajwa kuwania saini ya Ntibazonkiza, ambaye msimu uliopita alitwaa Ufungaji Bora akipachika mabao 17, sawa na aliyekuwa Mshambuliaji wa Young Africans aliye Misri kwa sasa sasa, Fiston Mayele.Msimamo wa Saido ni Miaka miwili huku Msimamo wa Uongozi wa Simba kutokana na Umri wake wapo ukiwa kuendelea nae endapo atakubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja tu.