TAARIFA za kuaminika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa kiungo wa timu hiyo Saido Ntibazonkiza amegoma kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo.
Simba wanamtaka asaini mkataba wa mwaka mmoja ambapo inaelezwa kuwa yeye anahitaji kupewa mkataba wa miaka miwili ili asalie hapo.Na Kama Simba watashundwa kumpa miaka miwili yupo tayari kuondoka kwenye dirisha hili huku akiwa anatajwa kuwindwa na timu nyingine ambazo zinahitaji saini yake kutoka Rwanda na Burundi.
Saidoo Ntibazonkiza amekuwa na Utaratibu wa kuhitaji miaka miwili kwenye Kila mkataba wake mpya, Hilo linatajwa pia kumuondoa Yanga Msimu wa mwaka juzi.