ZAHERA AIBUKIA NAMUNGO

Klabu ya Namungo imemtambulisha Mwinyi Zahera kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Baada ya aliyekuwa Kocha wa Timu hiyo Denis Kitambi kutimkia Geita Gold FC.

Namungo kutokea mkoani Lindi, imemchukua Zahera ambaye ana uzoefu na ligi ya Tanzania akizinoa klabu za Yanga, Polisi Tanzania na Coastal Union kabla ya kujiunga na Namungo.

Namungo ipo nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Ligi Kuu tayari imecheza mechi 14 ikishinda mechi 4, kufungwa 5 na droo 5 na ina pointi 17.

Acha ujumbe