Zahera Kocha Mpya Polisi Tanzania


Aliyekua Kocha wa Yanga SC na baadae Mkurugenzi wa soka la vijana na wanawake wa klabu hiyo Mwinyi Zahera amejiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Polisi Tanzania hadi mwisho wa msimu kwa mkataba wa miezi 6.

 

Zaheri Kocha Mpya Polisi Tanzania

Klabu ya Polisi Tanzania imemtambulisha kocha huyo huku akienda kuichukua timu hiyo ambayo ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo baada ya kucheza michezo yao 14 na kushinda mbili tu.

Polisi Tanzania katika hiyo michezo ameenda sare mara tatu tu huku akipoteza michezo yake tisa na kujivunia pointi tisa peke yake.

Zahera anatarajiwa kuja kubadilisha timu na matokeo yao kwa ujumla wanayoyapata huku mkataba wake aliopewa unaweza kutamatika au kuendelea kutokana na matokeo ambayo atayapata.

Zaheri Kocha Mpya Polisi Tanzania

Mechi inayofuata ya Polisi watakuwa nyumbani kukipiga dhidi ya Azam FC ambao wapo katika nafasi ya 2 wakiwa na pointi zao 32 huku ikiwa ni mechi ya kwanza ya Zahera kuona atafanya nini katika timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.