INAELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kumtangaza kiungo Augustin Okrah raia wa Ghana kesho Jumapili baada ya kuinasa saini yake.
Nyota huyo anatajwa kuwa kwenye hesabu za mwisho kumalizana na mabosi hao kwa ajili ya kuanza changamoto mpya.Okrah aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba alikwama kuonyesha uwezo wake kwa wakati huo mpaka alipokutana na Thank You.
Habari zimeeleza kuwa Yanga wamemuandalia mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kupata huduma ya winga huyo mwenye kasi akiwa na mpira uwanjani.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wanatambua uwezo wa Okra hivyo kama watapata saini yae basi itakuwa ni jambo la kuwatambulisha kwa Wananchi.“Mchezaji ambaye anapata nafasi ya kucheza Ghana na kuitwa timu ya taifa ina maana kwamba huyo sio mdogo ni mkubwa ni suala la kusubiri,”