OFISA Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kuwa, wanatarajia kuanza kutambulisha wachezaji waliowasajili dirisha dogo mwishoni mwa mwezi huu.
Ambapo kuna jina la mchezaji mkubwa wamepanga kulitambulisha Desemba 31.“Mchezaji atakaetambulishwa siku ya tarehe 31 mwezi huu pale Zanzibar atafunika show aliyoifanya Diamond hapo jana ilikuwa ni show kubwa ya kimataifa lakini kwa mchezaji huyu ataifunika,”“Siku hiyo tunakwenda kumtambulisha mgeni mwenyeji,ni mgeni lakini mwenyeji na ninavowajua waandishi wa habari wanavojua kutegeshea, wanasubiri tufike bandarini waanze ku zoom nawaambia wameshachelewa, na nilijua hilo mapema kwahiyo tulishampeleka Zanzibar mpaka sasa yupo huko,” alisema msemaji huyo wa klabu ya Yanga