Tuzo ya kocha bora msimu kunako ligi kuu ya Uingereza itawaniwa na makocha watano, Lakini mchuano mkali unatarajiwa kua baina ya makocha wawili ambao ni Pep Guardiola na Mikel Arteta.
Makocha ambao wanawania tuzo ya ya kocha bora wa msimu mbali na Mikel Arteta na Pep Guardiola, Lakini makocha wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Andoni Iraola wa Bournamouth, Jurgen Klopp wa Liverpool, pamoja na Unai Emery wa klabu ya Arsenal.Makocha hao wanaowania tuzo ya kocha bora wa msimu ndani ya ligi kuu ya Uingereza wamekua na msimu bora sana ndani ya msimu huu, Huku vilabu vyao vikiwa vimefanya vizuri pia kwenye ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa.
Kocha kama Andoni Iraola amefanikiwa kufanya kazi kubwa sana ndani ya Fc Bournamouth, Lakini pia Unai Emery amefanya kazi kubwa sana ndani ya klabu ya Aston Villa na kuiweka kwenye nafasi nne mpaka sasa bila kumsahau Jurgen Klopp ambaye amekua kwenye nafasi ya kuwania ubingwa mpaka sasa.Pamoja na makocha wengine kufanya vyema kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu, Makocha Mikel Arteta wa Arsenal na Pep Guardiola wa Manchester City ndio wanatajwa kama kua na nafasi kubwa zaidi ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na ushindani ulipo baina ya vilabu hivo mpaka sasa kwenye wakichuana kuwania taji la ligi hiyo.