Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland kuwania mchezaji bora wa msimu wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa pili mfululizo.
Mshambuliaji Haaland hatakua mwenyewe kwenye kinyang’anyiro hicho kwani kwani wachezaji wengine kadhaa nao watakua wakigombania tuzo hiyo ambao ni Decline Rice wa Arsenal, Phil Foden Man City, Virgil Vin Dijk Liverpool, Martin Odegaard Arsenal, Cole Palmer Chelsea, Ollie Watkins Aston Villa, na Alexender Isak wa Newcastle United.Mshambuliaji huyo wa klabu ya Man City ana msimu wa pili kwenye ligi kuu yas Uingereza lakini ameonesha ubora mkubwa ambao unamfanya mpaka sasa kuwania tuzo yake ya pili ya mchezaji bora wa msimu, Kwani msimu uliomalizika yeye ndio alitwaa tuzo hiyo pamoja na kuisaidia klabu yake kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.
Ubora mkubwa ambao mchezaji anakua anauonesha ndio unamfanya kuingia kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu, Huku Haaland amekua akifanya hivo kwa msimu wa pili sasa kwani mpaka sasa anaongoza kwenye orodha ya mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza.Wachezaji wengine pia waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo wamekua na msimu bora sana ndani ya vilabu vyao, Jambo ambalo limefawafanya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu kunao ligi kuu ya Uingereza.