Leo inapigwa nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani ulaya pale kwenye dimba la Santiago Bernabeu kati ya mabingwa wa ligi kuu ya Hispania klabu ya Real Madrid dhidi ya klabu ya Fc Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani.
Mchezo kati ya Real Madrid na Bayern Munich ni mchezo wenye hadhi kubwa sana barani ulaya haswa kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya mpaka kufikia kuuita (European Clasico) Hivo mchezo wa leo utakwenda kua mchezo mgumu na wenye kuvutia kwelikweli kwa wapenzi wa soka ulimwenguni.Mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa katika dimba la Allianz Arena ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Kwa maana hiyo mchezo wa leo ni kama unaanza upya kwani kila timu ina nafasi ya kufuzu hatua ya fainali japokua miamba ya soka nchini Hispania inapewa nafasi kubwa zaidi kufuzu.
Klabu ya Bayern Munich wakifanikiwa kutinga hatua ya fainali basi watakwenda kukutana na ndugu zao klabu ya Borussia Dortmund ambao jana wamewatupa nje klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Lakini pia historia itakua inajirudia kwani mwaka 2013 timu hizo kutoka Ujerumani zilicheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya katika dimba la Wembley ambalo fainali itapigwa pia mwaka huu.Klabu ya Real Madrid wamekua na historia nzuri sana kwenye michuano ya ulaya kwnai ndio mabingwa mara nyingi zaidi kwenye michuano hiyo, Lakini Bayern Munich ni moja ya klabu mbili za mwisho kuitoa Real Madrid katika uwanja wake wa nyumbani wakifanya hivo mwaka 2012 kwenye hatua hii pamoja na Ajax waliofanya hivo mwaka 2019 hivo klabu hiyo ina nafasi ya kuishangaza dunia licha ya kutopewa nafasi kubwa.