YANGA YAFUNGUKA ALICHOJIFUNZA C.E.O TP MAZEMBE

BAADA ya mijadala kuwa Mingi juju ya nini kimemfanya C.E.O wa TP Mazembe Fredric Kitengie aje kujifunza kutoka Yanga, licha ya kuwa Mazembe wameizidi Yanga Kila kitu, uongozi wa Klabu hiyo imekuja na majibu.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa, Kitengie hakuja Yanga kujifunza jinsi ya kuchukua Ubingwa kama watu wanavyofikiria.yangaBali, amekuja kujifunza vitu vingi tofauti ikiwemo uongozi bora, ukuaji wa haraka wa Klabu na namna ambavyo timu hiyo imeamini kupitia vijana na mambo mengine mengi ambayo siyo Lazima watu wajue.yangaKamwe ameongeza kuwa, Kitengie ameshangazwa na namna ambavyo timu hiyo inaendeshwa na kwake imekuwa ni Faraja kubwa kupata alichokitarajia na zaidi.

Acha ujumbe