Kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes ambaye anafundisha klabu ya Westham United kwasasa anatarajiwa kutimka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Klabu ya Westham mpaka sasa imeshaamua kuachana na kocha David Moyes mwishoni mwa msimu huu, Jambo ambalo litamfanya kocha huyo kutafuta changamoto kwenye klabu nyingine.Klabu ya Westham inaelezwa kua kwenye mazungumzo na kocha wa kimataifa wa Hispania Julen Lopetegui kwajili ya kuchukua kibarua cha kuinoa timu hiyo kuelekea msimu ujao baada ya kuachana na kocha huyo Mskochi.
Klabu ya Westham ilifanikiwa kufanya vizuri msimu uliomalizika na kutwaa taji la michuano ya Uefa Conference league, Hivo viongozi wa klabu hiyo walitarajia makubwa zaidi msimu huu lakini mambo yamekua tofauti na ndio sababu ya kuamua kuachana na kocha huyo.
Klabu ya Westham imepokea kichapo cha mabao matano kwa bila leo mbele ya klabu ya Chelsea ikiendelea kuchochea moto kwa kocha David Moyes kutimka, Kwani msimu huu mambo yamekua tofauti kwa upande wake tofauti na msimu uliomalizika.